VIKWAZO VYA KUFIKIA HATMA YAKO na Mch. Mwangasa (SNP, Ufufuo Na Uzima, MOSHI)
Jumapili.. Tarehe 13/5/2012
Somo: Vikwazo Vya Kuzuia Hatma Yako (HOFU)
SNP Mwangasa |
Utangulizi:
Hesabu 13:17-> , Musa aliwatuma watu 12 wakachunguze nchi, waliokuwa
ameahidiwa. Na baada ya kuichunguza nchi kila mmoja akaja na majibu. Wakaeleza
mambo mazuri katika ile nchi, kwamba kuna maziwa na asali, lakini wakaja na
taarifa nyingine kuwa nchi inakula watu na kuna wanefiri.. Tunaweza kutambua
kirahisi kuwa hawa watu walipo waona waliingia kwenye hofu.. kumbe hofu yaweza
kuhatarisha hatma yako..
Nguvu ya Milango ya Fahamu katika
kuleta hofu
Binadamu ana milango ya fahamu mfano
macho, pua, masikio n.k. vitu hivi vyaweza kutumika kumtukuza Mungu au
kukukatisha tamaa,
i) HOFU KWA KUONA
kimsingi watu hawa waliingiwa na hofu kwasababu ya macho yao.. na haya macho yakawafanya wasahau yote ambayo Mungu aliwatendea hapo kwanza. Walisahau jinsi Mungu aliwavusha bahari ya shamu.. kumbe hata kwenye maisha ya kawaida Mtu unaweza kusahau matendo makuu ya Mungu aliyowahi kukutendea. Kwasababu tu ya hofu, kumbe hofu yaweza kukufanya ukose hatma yako..

ii) HOFU KWA KUSIKIA
Baada ya hawa watu kurudi, kutoka kutazama wakaja na taarifa mpya, katika wale 12, 10 wakasema yale mambo ya kukatisha tamaa, na makutano walivyosikia waka vunjika moyo. Na hii ikawapelekea kukata tama na kutaka kuwapiga mawe Kalebu na Joshua ambao walisema kuwa Mungu aweza kuwaokoa na watu wale. Kumbe Hofu yaweza kuingia kwasababu ya kusikia.. na ikakupelekea ukate tama ya kuishi na hivyo kuharibu hatma yako.

Nguvu ya taarifa;
Taarifa yaweza kukufanya urudi nyuma
kwa kuingiwa na hofu, wana wa Israel nao waliingiwa na hofu, hadi wakanena
maneno ya makufuru. Kumbe taarifa ni za kuzitilia maanani taarifa yaweza
kumfanya mtu atende dhambi ya hofu (kwa maana biblia inasema kuwa kila jambo
linalotendwa pasipo imani ni dhambi,) hofu ni dhambi.
Mch. Mwangasa akiwaondolea vikwazo kufikia hatma yao |
Madhara ya Hofu
Hofu yaweza kukusababisha kutokujiamini, kukata tamaa, inavunja nguvu ya imani, kurudi nyuma, kuishiwa nguvu, kuchoka na unaweza kutamani kujaribu njia nyingine ambayo ni mkato. Hofu ni mwanzo wa kushindwa. Mfano: Kuna mtu alikuwa na mgodi ambao aliuchimba miaka mingi lakini hakupata dhahabu na miaka ilipokwenda akaamua kuliuza kwa kupata hofu kuwa miaka itapita na ataliacha kuwa halina kitu. Siku chache baada ya kuliuza, akapita mgodini akamkuta Yule mtu aliyemuuzia anapakua dhahabu, baada ya kumuuliza akamwambia , nakushukuru sana maana baada tu ya kuniuzia mgodi sikulazimika hata kutumia mashine. Maana dhahabu zilikuwa dhahabu.

Kumbe wakati mwingine hofu yaweza
kukufanya ukate tamaa wakati unakaribia kwenye hatma yako. Wana wa Israel
walipoisikia ile habari wakaamua kulia usiku kucha, na kuunza kusema bora Mungu
angewaacha kule Misri, hii yote ni kwasababu hofu walizozipata kutoka kwenye
taarifa ya wapelelezi 10.
Nguvu ya Ujasiri
Esta 5:1-> .., Ilipotangazwa amri
kuwa wana wa Israel wauwawe, Esta ahakuogopa bali walichukua hatua ya kuomba na
kuchukua hatua ya kwenda kwe mfalme kinyume na desturi. Huu Ujasiri wa Esta
ukawaokoa kutoka katika kuangamia kumbe kuna uweza katika ujasiri. Mungu
hakutuumbia roho ya uoga.
Joshua 3 :1->.., wana wa Israel walipofika karibu kabisa ya kanaani. Hili neno *karibu kabisa* ni la muhimu likimaanisha walikuwa karibu na hatma yao. Na inawezekana umekaribia kufika karibu na hatma yako, ndipo wakakutana na mto Yordani wakpata hofu kwa vile mto ulikuwa umefurika, na wakasahau kuwa Mungu aliwavusha kwenye bahari.. ya shamu.

Kumbe waweza kukaa unamtukuza Mungu
na matendo yake makuu na ukataja uweza wake, na kusimulia matendo makuu lakini
hofu ikikuingia tu hayo yote utayasahau. Hofu yaweza kukusahaulisha uweza wa
Mungu aliokutendea. Lakini jambo la ajabu likatokea, ujasiri wa Joshua
ukawafanya kuvuka tena kwa kukanyaga maji yakiwa yanatembea.
Mch. Mwangasa akihubiria maelfu |
Ushindi Juu Ya Hofu.
Ukishinda hofu moja kwa moja
unaondoa vikwazo kwa hatma yako na Baraka zetu. Mungu ametupa kushinda dhambi
ya hofu.. na ndio maana ni vizuri toks motto akiwa mdogo kusikia maneno mazuri
ya kumletea ujasiri na si kumtia hofu na kumkatisha tamaa. Mungu
ametutengenezea hatma njema lakini lakini hofu yaweza kutuondoa kwenye hatma
hii..
Wana wa Israel walibeba sanduku la agano ambalo ndani yake kulikuwa na vitu vyenye kumbukumbu ya uwez a wa Mungu. Hivyo hata sisi tuna wokovu ndani ya wokovu kuna Jina la Yesu na ndani kuna uweza na ujasiri kumbe ujasiri wetu unatoka kwenye jina la Yesu ndani ya wokovu.
Mungu akubariki.

0 comments:
Post a Comment