MTU WA IMANI
Na Mch. MWANGASA (Snp, Ufufuo na
Uzima, Moshi)
Tarehe : 9/12/2012
Snp Mwangasa |
Utangulizi :
Warumi 4:13; Ibrahimu aliitwa na Mungu kutoka nchi aliyokuwepo
(Uru ya wakaldayo), Mungu akamuahidi kuwa atakuwa baba wa mataifa (uzao wake
kama mchanga wa bahari). Lakini ikapita miaka bila Ibarahimu kupata mtoto, na
kwa hali ya kawaida angeweza kukata tamaa.
Kupitia habari hii, tunajifunza mambo matatu:-
1.
Ibrahimu hakuangalia
udhaifu wa kutokuzaa bali aliangalia Ahadi ya Mungu.
Kuna wakati wa kuangalia jambo ambalo Mungu amekuahidia. Neno la
Mungu ni ahadi za Mungu kwetu. Na ndio maana alipoona uzee na hata tumbo la
Sara mkewe. 19-20’ “Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali
ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama
miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara. Lakini
akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani,
akimtukuza Mungu;”
2. Pamoja na jambo hilo, Ibrahimu pia aliangalia
uweza wa Mungu.
Snp Mwangasa akihubiri Kawe |
Kuna wakati mwingine majina ya vitu yanaweza kukutisha, aidha
kwa kuangalia desturi au asili. Kama Ibrahimu angeangalia
desturi asingetarajia kupata mtoto katika wakati ule. Katika Mstari 21’ “huku
akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.” Ibrahimu
aliangalia uweza wa Mungu anayemwamini.
Mtu wa Imani huwa anaangalia anapokwenda, na sio
anapotoka. Warumi 4:17 “(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa
mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha
wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.” Mungu
anayataja mambo ambayo hayapo, yaani yajayo kama yapo nah ii ndio tafsiri ya
Imani. Na ndio maana; ingawa Mungu haonekani kwa macho lakini hilo halimfanyi
asiwepo. Mtu mwenye Imani aangalii yanayoonekana bali yasiyoonekana. Mtu mwenye
Imani hata kama ameambiwa kuwa ni tasa yeye anakwenda kununua kitanda cha
mtoto. Hama kutoka katika kuangalia yaliyopo bali angalia kwa kufuata imani.
3. Ibarahimu aliamini kwa kutarajia, lisiloweza
kutarajiwa.
Majeshi ya Bwana wa Kawe wakisiliza injili |
Warumi 4:18 “Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili
apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao
wako.” Usiogope
kutarajia makubwa, Mungu anaweza kutenda yaliyo makuu mno. Kuna hazina zipo
gizani ambazo imani pekee ndio inaaweza kuzichukua. Ibrahamu kilichomfanaya
atarajie yaliyo makubwa Ni kwasababu aliiangalia ahadi ya BWANA. Hata sisi
hatujaletwa duniani kwa hasara. Mungu anakusudi la sisi kuwepo hapa duniani.
Yawezekana unapita katika wakati mgumu, lakini unachotakiwa ujue
ni kwamba, Mungu anaweza kutenda kwako ambayo watu wengi hawayatarajii. Swali
la kujiuliza.. “Unatarajia jambo gani?” Tafakari na uchague kuwa mtu
wa Imani: ili uweze kuwa mtu wa imani jifunze kuangalia kwanza uweza wa Mungu
kabla ya uweza wako mwenyewe.
Miliki Milango yote ya Baraka maana sisi ni wa Uzao wa Ibrahimu:
Mwanzo 13:14 “Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa
macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na
wa mashariki na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao
wako hata milele.”
Miliki ahadi ya Mungu kwetu…
0 comments:
Post a Comment