GLORY OF CHRIST

Genesis 1:28. God blessed them and said to them, “Be fruitful and increase in number; fill the earth and subdue it. Rule over the fish in the sea and the birds in the sky and over every living creature that moves on the ground..

Sunday, April 24, 2016

MAOMBI YA KURUDISHA NYOTA ILIYOFUNIKWA

Na SNP King Mwangasa.                                                                         
Ni rahisi mtu kujiuliza kurudisha nyota tena? Kulikoni mpaka kurudisha nyota?
Unajua nyota kwenye biblia inamaanisha kipawa cha mtu au inawakilisha kipawa cha mtu ambacho ndiyo dira na mwelekeo wa maisha ya mtu. Katika ulimwengu wa roho kila mtu ana kiashilia kinachoonyesha maisha yake na kiashilia hicho ndicho huitwa nyota. Kila mtu aliyezaliwa, amezaliwa kwa kusudi na hata kama njia iliyotumika kumleta duniani mtu huyo tunaiona si sahihi machoni petu lakini bado Mungu aliruhusu njia hiyo kumleta mtu maalumu duniani ili atimize kusudi lake.

SNP King Mwangasa akifundisha
 Mwanzo 37:5-
Yusuph alipoota ndoto ya kwanza kuhusu mganda wake kusimama katikati na ya kaka zake kumwinamia tunaweza kusema kweli hapa wivu una sababu kwa nini miganda yak ka zake imwinamie yeye? Na katika ndoto ya pili anaota nyota 11, jua na mwezi vinamwinamia, matoko a ndoto hii anachukiwa zaidi na baba anamkemea. Hapa suala si nyota wala mwezi na jua tuvionavyo angani? Ukali huu wa baba(Yakobo mtumishi wa Mungu, Yule aliyesema na Mungu baada ya kutia mafuta kule Betheli, aliye baba wa Israel wote) na chuki za ndugu zake ni kuhusu uelekeo wa maisha yao, kipawa. Yakobo aliyajua haya, alipata tafsri sahihi na ndo maana akayahifadhi.

Mathayo 2:1-10.
Walitoka mamajusi(wajuzi wa nyota) wa mashariki wakafika mpaka ikulu na kumuuliza “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia” Jambo la ajabu sana kwamba Yesu ambaye ni baba yetu, ni jina halisi la Mungu, mwokozi wetu, Eti alipozaliwa kuna kitu kilichotambulisha kuzaliwa kwake, hata hawa wachawi(Magi au Astrologers ) wakaona tokea mashariki ya mbali yaani watu tokea china au Thailand pengine au Japan nyota ya Yesu kabla hata hajazaliwa wakasafiri kwa ngalawa za kusukumwa na upepo pengine kutokana na tekinolojia ya wakati huo mpaka wakafika Yerusalemu kwa wakati. Haiishii hapo wamemkuta mfalme Herode badala ya kumsujudia yeye bado wanauliza habari za katoto kalikozaliwa na wanadiriki kusema wanataka kumsujudia. (Kinachowalazimisha kusujudu ni Nyota) Hawa si wajinga, ni wataalam hawa katika ulimwengu wa roho wanajua wanachokifanya.

Kumbe kama Yesu alipozaliwa alikuwa na nyota yake, vivyo kila aliyezaliwa ana nyota yake.
Kwa nini basi hawa mamajusi wa mashariki waende kumsujudia mtoto tu? Mfalme Herode alikuwepo hapo, haikutosha kumsujudu yeye? isitoshe huko walikotokea kuna wafalme pia kwa nini wasiwasujudie hao na kuridhika kama suala lilikuwa ni kuwasujudia wafalme? Jibu ni hili, kwa kawaida wachawi, wanga, wasomanyota na watu wote wa giza hupata nguvu kwa shetani ambaye ni kiongozi mkuu wa falme zote na mamlaza za giza. Kuzaliwa kwa Yesu Kristo, nuru iliangaza ulimwenguni mwote, giza likakosa nguvu(Yoh1:4b-5), kulitikisa kila falme zote na kusababisha taharuki katika ufalme wa shetani. Watu hawa walitafuta ni nini kimepelekea kukosa nguvu, wakajua kuna mfalme wa wayahudi amezaliwa na alishanenwa katika ulimwengu wa roho, ana uweza na nguvu za kushinda miliki zote na kwa kuwa wachawi ni watu wa rohoni kwa upande wa giza, wakatafsiri na kujua hayo.

Watu wa rohoni upande wa shetan (Wachawi)  wanaweza kuiona nyota ya mtu tangu siku anapozaliwa. Wakiiona nyota wanajua nyota inawakilisha kipawa cha mtu.

KAZI ZA NYOTA/KIPAWA CHA MTU
1.Hufanya mtu kuwa mahiri katika utendaji (Effectiveness)
2.Humfanya mtu kuwa mbunifu(Creative) 
3.Kipawa humsaidia mtu kutenda kwa ufanisi (Efficiency)
4.Nyota au kipawa huleta mvuto, watu huvutiwa na wewe (attraction)
5. Inasababisha mtu akubalike  kupata kibali (Divine Acceptance/fever )
6. Kinamfanya mtu awe jasiri  ujasiri wa kile, humpa mtu ujasiri wa jambo analolifanya (Divine Boldness)

Niishie kwa hayo machache, kwamba nyota ya mtu inapokuwa iko pamoja na yeye, na ikiwa nyota ya mtu imefunikwa inasababisha mambo hayo yasitendeke juu yako.
Mungu alivyotuumba anataka tuwe na ufanisi, umahiri, ubunifu, kibali, ujasiri na mvuto katika kutenda.

 Shetani yeye kumbuka ni kerubi afunikaye (Ezekiel 28:14) na hata sasa anatumia hila zake kufunika mema ya watu. Kuna matatizo yanaanzia siku mtu anapozaliwa kwa maelekezo na hila za shetani. Wapo waliofunikwa nyota zao na wazalisha kama yule mzalishaji wa Peresi na Zera na wengine waliacha hai. (Mwanzo 38:27-30, 1 Nyakati 27:2,3 Nehemia 11:6, Kutoka 1:15-17) Zera maisha yake yalitokana na kitu alichokifanya mzalishaji wao, wengine walioachwa hai pamoja na vipawa vyao kama wazalisha wa waebrania waliogoma kutekeleza amri ya farao na hatimaye wakawahifadhi hai pamoja na Vipawa vyao. Pia mavazi ya kwanza kazivaa au zawadi unazopewa vyaweza tumika kufunika maisha ya mtu. Siku mtu anapozaliwa anaweza kufunikwa nyota ya maisha yake, maana uhai unaanzia siku mimba inapotungwa na maisha ya mtu yanaanzia siku anapozaliwa na katika mda anapokuwa humo tumboni anakuwa salama, lakini siku unazaliwa mlinzi aliyekuwa akikulinda tumboni placenta (kondo) hubakia kwa mzalisha. Mzalisha anaweza kumtumia huyo mlinzi katika ulimwengu wa roho na kuyaharibu maisha ya mtu.

Ezekiel 16:4,5.
Ezekiel anawatabiri Israel siku alipozaliwa na katika kukua kwake. Shetani anawinda maisha ya mtu tangu day one. Shetani anafunika kipawa hukohuko rohoni kwa kuwa nyota au kipawa hakiko mwilini. Na mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba iitwayo mwili. Roho ndiyo mmliki wa kipawa na inatumia mwili kudhihirisha kipawa, hivyo shetani anafunika rohoni ili kisijidhihirike katika mwili.

Isaya 47:12-15.
Wachawi, waganga na wasomanyota wanashirikiana kufunika nyota na wanaweza kuharibu maisha ya mtu. Faraki ni elimu ya uchawi. Watu awa aina hii wote ni mtandao wa shetani.

Mhubiri 9:11
…. si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Ukifunikwa nyota yako wakatia wa bahati yako ukifika wanapewa wengine.

Isay 42:22


Chukua hatua sasa tuombe pamoja kwa mamlaka, tumwambie shetani toka na uachie nyota yangu, maisha yangu yachanue tena maana kwa kusudi hili mwana wa adamu alidhihirishwa ili azivunje kazi ibirisi, naye ndiye nuru ya watu na nuru yake yang’aa gizani wala giza halikuiweza, nawe hira zote za giza zisikuweze, kitu cha thamani alichokuumbia Mungu kionekne kwako katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Mamia ya watu wakisikiliza ujumbe wakati alipokuwa akihubiri SNP King Mwangasa






Platform Ministry wakiongoza mamia ya watu kwenye ibada yasifa na kuabudu
Wakati wa maombezi






0 comments:

Post a Comment

Prayers (Andika Maombi yako Hapa)

Name

Email *

Message *

Sponsor

Kama unapenda kuchangia Huduma Yetu Tafadhali wasiliana nasi