SOMO:
KURUDI KWENYE KUSUDI LA MUNGU LA MILELE
RP Adriano akifundisha ndani nyumba ya ufufuo na uzima Moshi |
Na
RP Adriano.
Kila
mtu ana kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yake, ambalo ndilo limebeba maana
ya yeye kuishi na ukiondoa kusudi unaondoa maana ya yeye kuishi na ukimuua mtu
huyu unakuwa umeharibu kusudi.
Kutoka 4:19 “Bwana akamwambia Musa huko Midiani, Haya, nenda, karudi Misri; kwa
kuwa wale watu wote waliokutaka uhai wako wamekwisha kufa.”
Waebrania 11:23- “Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake,
kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme. Kwa
imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; akaona ni
afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika
dhambi kwa kitambo; akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu
kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. Kwa imani akatoka
Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye
asiyeonekana.”
Kwa imani Musa akakataa kuitwa mwana wa
Binti Farao, Musa alikuwa anaongea kwa imani na iwe hivyo kwako leo kataa kuitwa
maskini, kataa kuitwa tasa, kataa kuitwa mgonjwa, kataa kuitwa asiye na mbele
wala nyuma na kila jina unaloitwa kinyume na makusudi ya Mungu kwa kuwa
ulizaliwa kwa kusudi.
Baada ya kufa aliyeitafuta roho ya mtoto
Yesu (Herode), Yusufu aliambiwa arudi na Musa pia walipokufa Farao na viongozi
wake waliomtafuta aliambiwa arudi yaani akae akifanya anachotakiwa kukifanya,
arudi kwenye makusudi ya Mungu na kufanya kile anapaswa kukifanya.
Watu wakisikiliza neno la Mungu alipokuwa akihubiri RP Adriano Ufufuo na uzima Moshi. |
Tumeshambulia jana na kumumaliza
anayetafuta maisha yako na yote uyafanyayo na sasa leo tuendelee mbele, hapo
ulipo sasa KATAA KUONEWA, KATAA KUDHARAULIWA, KATAA KUIBIWA NA SHETANI MAWAKALA
WAKE KWENYE MAENEO YOTE YA MAISHA YAKO KIMAFANIKIO, na mambo haya tunayakataa
kwa imani yaani Rohoni nayo yanadhihirika katika mwili.
Rumi
10:17” Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la
Kristo.” Tunakwenda makanisani kusikia neno na tunasoma neno kwenye mitandao
imani yetu inajengwa na tunapata nguvu za kuharibu falme za giza na kurudi
kwenye makusudi ya Bwana yale aliyotukusudia maishani
Maandiko yanaonyesha Israel walipokuwa
utumwani walionewa na Mungu aliweka kusudi lake ndani ya Musa na shetani
alipotaka kumuua Musa ililazimikia afe yeye ili makusudi ya Mungu yatimie ndani
ya watu wake Israel.
Mwanzo 15:8-16 Maandiko yanaoonyesha kuwa
hiki kilitokea kwa sababu ilikuwa ni makusudi ya Mungu, na Ibrahimu aliagana na
Mungu mambo haya kwa hiyo isingekuwa rahisi kuharibu makusudi ya Mungu, na
kwako pia Mungu ana makusudi ya kufanya kupitia wewe hutakufa na itafikia
wakati watakuheshimu tuu maana itatokea bila wewe hawatafanikiwa kama
ilivyokuwa kwa Yusufu walewale waliomfunga walimtoa ili awatafusirie ndoto, awatawale,
awasaaidie.
Majeshi ya Platform yakimsifu Mungu ndani ya nyumba ya ufufuo na uzima Moshi |
Tuombe pamoja maombi haya, “KWA JINA LA
YESU KRISTO TUNAWAFYEKA WOTE WANAONIZUIA KUINGIA KWENYE MAKUSUDI YA MUNGU,
WAFYEKWE MAJOKA NA WATAWALA WOTE WANAO ZUIA MAKUSUDI YA MUNGU KWENYE MAISHA
YETU, KILA FARAO WA MAISHA YAKO NA AFE MWENYEWE KATIKA JINA LA YESU KRISTO WA
NAZARETH.
Katika jina la Yesu wewe ukaheshimiwe na
waliokuonea wakitaka kusafiri wakute we ndo mtoaji wa visa, wakitaka kupona
magonjwa yao wakakute we ndo mwenye dawa pekee ya shida yao, wakakuheshimu na
Bwana akakuinue kati ya wote ukajazwe kicheko badala ya huzuni na ukafurahie
makusudi ya Mungu kwako na yakatimie kwa jina la Yesu.
Amen.
0 comments:
Post a Comment