APOSTLE: JOSHUA
07/07/14
SOMO: MFUNGUENI AENDE ZAKE.
Yohana 11: 38-44, Marko 11:1-3
“Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. Yesu akasema, Liondoeni jiwe.
Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?
Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.”
Siku zote tatizo lina harufu
mbaya, ni kifungo na halivutii hata watu wapende kukufungua kama Yesu hakuwa
ndani ya mfunguaji. Lazaro akiwa kabrini hata dada zake walisita kulifunua jiwe
lililowekwa mlangoni ili kumsaidia. Mtu aliyefungwa anahitaji mfunguaji, nasi
tunaye Yesu afunguaye matatizo ya kila aina. Nguvu ya kufungua ametupa, “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa
mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni”
Mathayo 18:18
Hata hivyo ni vema kufahamu kwamba Gereza la namna
yoyote ambalo mtu anafugwa linahusisha vitu(maeneo) makubwa matatu,
ü
Bwana jela(Mfungaji au afungaye)
Bwana jela(Mfungaji au afungaye)
ü
Mfungwa(mtu, biashara ya mtu, huduma, ndoa, mafanikio,elimu n.k. )
Mfungwa(mtu, biashara ya mtu, huduma, ndoa, mafanikio,elimu n.k. )
ü
Gereza(mahali alipofungiwa)
Gereza(mahali alipofungiwa)
Mara nyingi watu wengi huombewa na
wakafunguliwa, lakini tatizo hurudi palepale kwa sababu watu wengi
hushughulikia tatizo na kuacha chanzo mfungaji(bwana jela) na kutochukua hatua
ya kutoka gerezani.
Na ndo maana hata mapepo hutoka na kisha husema tutarudia tena nyumba yetu na yakikuta imepamba yaani (imekosa neno, imeacha wazi bila ulinzi wa kiMungu kupitia maombi, haajafungwa malango yake kwa adui, mfungaji hajafungwa na aliyefungwa hajachukua hatua ya kutoka katika eneo la gereza alilomfungwa n.k.) bbKolosai 3:16 “Neno la kristo na likae kwa wingi ndani yenu….”
Mungu amesema atabariki kazi za mikono yetu ni kweli kabisa, ila ili tushinde na kuishi hali hiyo tunapaswa tufunguliwe mikono& miguu yetu, tumshinde mfungaji kabisa mfungaji, na kuliharibu gereza.
Isaya 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”
Tunamfunga kila afungaye, tunajifungua katika eneo lolote la maisha yetu lililofungwa(biashara, ndoa, kazi, kutoelewa, kukosa mtoto, kufeli kimasomo, kutoelelewa darasani n.k.) na tunaamru kila eneo lililomeza maisha yetu, limefanyika kuwa gereza na kila harufu mbaya katika ulimwengu wa roho, tufungua kwa damu ya Mwanakondoo. Tunatangaza uhuru katika maisha yetu kwa Jina la Yesu Kristo, imenenwa mwana akikuweka huru unakuwa huru kweli kweli.
0 comments:
Post a Comment