GLORY OF CHRIST

Genesis 1:28. God blessed them and said to them, “Be fruitful and increase in number; fill the earth and subdue it. Rule over the fish in the sea and the birds in the sky and over every living creature that moves on the ground..

Thursday, July 17, 2014

Kila tatizo lina chanzo chake, Na RP Adriano


SOMO: KILA TATIZO LINA CHANZO CHAKE

RP Adriano akisoma neno
Na. RP Adriano


Mhubiri 9:2, Kutoka 20:24, Mwanzo 22:1, Walawi 17:7
Kama ilivyo kwa vitu au mambo yanayofanyika katika ulimwengu wa mwili yana chanzo na ndivyo yalivyo mambo ya rohoni. Tatizo lako lina chanzo, shida ya mtu ina chanzo, ugonjwa unaomsumbua mtu una chanzo na kila kinachotokea maishani mwa mtu yeyote yana chanzo.

 Mambo yote yawatukia wote sawasawa; kuna tukio moja kwake mwenye haki na kwake asiye haki; kwa mtu mwema na kwa mtu mwovu; kwa mtu aliye safi na kwa mtu asiye safi; kwake yeye atoaye kafara na kwake asiyetoa kafara; kama alivyo huyo mwema ndivyo alivyo mwenye dhambi; yeye aapaye na yeye aogopaye kiapo.

Kafara ni sadaka ya mtu yenye lengo fulani kwa Mungu au kwa mashetani. Kafara zimekuwa zikitolewa tangu mwanzo baada ya Adamu kufukuzwa Eden na kumzaa Kaini na Abel walikuwa wakitoa na utaona Abeli anatoa wanyama na Kaini vivyo alikuwa akitoa sehemu ya mazao yake.
Nuhu alipotoka kwenye safina. Mwanzo 8:20Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
RP Adriano akihubiri

Ibrahimu alijaribiwa na Mungu amtoe Isaka mwanawe wa pekee kafara kwa kumchinja na kumweka juu ya madhabahu kuwa sadaka ya kuteketezwa. Na kuna wafalme/watawala waliowatoa wana kuwa kafara ili tuu washinde vita. Kwa mifanno hiyo michache unaweza kuona ni kwa kiasi gani kafara imekuwa ikifanyika na matokeo ya kafara.

Mungu aliagiza watu wamtolee dhabihu za kuteketezwa juu ya madhabahu(Kafara) Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng'ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia” Kutoka 20:24

Pamoja na kafara hizo Mungu pia alimtoa mwanawe awe dhabihu/kafara ya ukombozi kwa watu wote.

Watu wamekuwa wakitoa kafara kwa shetani wakiwapa waganga wa jadi ambao ni makuhani wa shetan ili wapate utajiri, watimize haja zao za kuwaona wengine wakiishi maisha ya magonjwa, umaskini, watoto wakifeli darasani, ndoa ikiharibika na kuharibu maisha ya watu au biashara; LAKINI leo katika jina la Yesu kila chanzo cha tatizo lako kinapigwa na kuharibiwa, naye aliyekubali kutumika kama chanzo cha tatizo hilo tunatuma moto na upanga wa Roho mtakatifu uwafyeke wote walisababisha matatizo yako, waharibiwe kabisa na kubakia kama makapi, Malaika watakatifu wa Mungu wawashambulie popote walipo na kuwaharibu kabisa.
Umati wa watu wakisikiliza mahubiri ya neno kanisani Ufufuo na uzima Moshi wakati RP Adriano akihubiri.

Jambo moja kwa mtu mwenye Mungu ni kwamba Mungu ni mwenye haki juu ya maisha yao na hapo hata watu wakakutengenezea matatizo au shida yeye atasimama kama mwenye haki juu yako.

Yesu alipowatuma wanafunzi wake aliwaambia mtamkuta mwanapunda amefungwa mfungueni na mtu yeyete akiwauliza mwambie Bwana ana haja naye. Na ndivyo itakavyokuwa kwako wewe uliyefungwa hatubabaishwi na atuulizae kwa nini unarudisha wafu kuwa hai, kwa nini unawaombea hawa kupona, au kwa nini unawafunguwa hawa? Jibu letu ni moja tuu kwamba Bwana ametutuma kuwafunguwa waliofungwa na kuwaweka huru, walio mashimoni watolewe, walioibiwa warudishwe na waliofungwa na vifungo vya namna mbalimbali wawekwe huru kwa jina la Yesu kristo wa Nazareth.

Tunatangaza leo katika jina la Yesu kila kafara za damu juu ya madhabahu na popote tunazikanyaga na kila madhara yake tunayaharibu katika jina la Yesu Kristo Ubakie huru na ufanikiwe sawa na makusudi ya Mungu juu ya maisha yako, pokea hakima yako, biashara yako ifanikiwe, ulishushwa na watu uinuliwe, uliyeonewa pokea utetezi wako kwa jina laYesu Kristo AMEN.
Ubarikwe.



0 comments:

Post a Comment

Prayers (Andika Maombi yako Hapa)

Name

Email *

Message *

Sponsor

Kama unapenda kuchangia Huduma Yetu Tafadhali wasiliana nasi