NENO: NIMECHOKA KUVAA MAGUNIA.
AP Hosea akihubiri ibada ya ijumaa jioni 4 July 2014 |
Na AP Hosea Shaban
Zaburi 35:1-14
“Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana
nami.
Uishike ngao na kigao,
Usimame unisaidie.
Uutoe na mkuki uwapinge
wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.
Waaibishwe,
wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe,
Wanaonizulia mabaya.
Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha
chini.
Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa Bwana akiwafuatia.Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia
shimo nafsi yangu…………….”
Somo hili
linaonekana la ajabu, hasa kwa sababu ya kichwa cha somo chenyewe kwamba
tunavaa magunia hali tunaonekana tumevaa nguo Lakini katika hali ya huzuni,
kuteswa na ugumu tunaokutana nao umebeba hali ya mtu aliyevaa magunia, (aombolezaye,
asiye na furaha, aliyetengwa, asiyeishi katika matarajio yake na mwenye huzuni,
aliyetengwa hata na marafiki zake n.k)
Lakini
leo kuna habari njema kwa yeyote alionewa, aliyeishi maisha ya kupigana na
kuishia kulia na umekosa furaha juu ya maisha yako “KWAMBA
BWANA YUPO LEO ILI AKUPIGANIE ATETE NAO WANAOTETA NAWE NA KUKUPA UHURU WAKO”.
Amesema “Njoni kwangu, ninyi
nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira
yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi
mtapata raha nafsini mwenu.”
Ni
saa yako ya kulichoka tatizo lako, ukatae kuendelea kuishi na ugumu huo
ulioupitia kwa mda mrefu, useme sasa basi kuvaa magunia haya ya (kukosa mtoto, kuugua
kila mara na mwili wako kuwa nyumba ya magonjwa kwa kuzuruumia afya,
kusimangwa, kuchekwa, kudharauliwa, kufedheheka, kuaibishwa na kuishi kwa
machozi siku zote) na iwe zamu yao leo walionitega, wajinase wenyewe kwenye
mitego yao, wanaopenda kuona nikilia walio wenyewe, Tunafanya vita dhidi yao,
Bwana atete nao, wapigwe kabisa, waaibishwe, wafedheeshwe, njia zao ziwe giza
na utelezi, malaika wa bwana akiwafuatia nyuma, wawe kama maakapi hata
wakomeshwe kabisa.
Yavue magunia ya dhiki, kuonewa,
kuaibishwa, kushindwa na uvikwe vazi la furaha
Mambo
haya na yatendeke kwako na upokee ukombozi kamili katika jina la Yesu Kristo
Ameni.
0 comments:
Post a Comment