GLORY OF CHRIST

Genesis 1:28. God blessed them and said to them, “Be fruitful and increase in number; fill the earth and subdue it. Rule over the fish in the sea and the birds in the sky and over every living creature that moves on the ground..

Friday, July 18, 2014

Kila tatizo lina chanzo, na RP Adriano, Ibada ya Ijumaa jioni


RP Adriano akihubiri

SOMO: KILA TATIZO LINA CHANZO CHAKE.

Na. RP Adrian

……. Limeendelea kutokea jana.

Kumbukumbu 8:18, 1Petro 2:2, Yohana 3: 3
Jana tuliongelea kafara kama chanzo kimojawapo cha matatizo na leo tutaendelea na kugusia ndoto pia.
Watu hutoa kafara ili kupata nguvu za kupata madaraka, kutawala, utajiri n.k.
Ili mtu afanikiwe lazima aanze na roho yake kwanza, na mambo yanatokea yakianzia rohoni, na Yohana anasema
“Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”
3 Yohana1:1-2.

Wachawi wanajua namna ya kuutumia vizuri ulimwengu wa roho kupitia uchawi na hujigeza maumbo. Watu huota ndoto wakifukuzwa au wakipigwa na vitu au wanyama wakidhani kuwa ni ni ndoto tuu, kumbe viumbe vya kiroho kama majini na watu halisi ndio hujibadili na kuvaa maumbo hayo ili wasitambulikane na kutimiza azima yao kwa urahisi.
Leo ndoto zimekuwa chanzo cha matatizo mengi kwenye maisha ya watu, na ndo maana utasikia mtu anasema aliota ndoto fulani mbaya na ugonjwa ukamuanza, au aliota mtu kamnyang’anya kitu fulani na biashara yake ikafirisika. Chanzo ni ndoto na kwa kushindwa kufanyia kazi ili kuharibu chanzo hicho maisha ya mtu yakaharibiwa.
Umati wa watu wakisikiliza mahubiri mapema jana akihubiri RP Adriano
Kwako leo tunatangaza ukombozi wako, na ni saa ya ufufuo na uzima juu ya familia yako, biashara yako, kazi iliyokufa na ifufuke kwako kwa jina la Yesu Kristo.
Yesu alisulubiwa na wakamzika kaburini, wakasema tumemuweza, hatatupa shida tena kwenye miji yetu, hatawafufua tena tuliowaua, hatawafungua tena tuliowafunga LAKINI SIKU YA TATU tuu AKAFUFUKA na alitokea malaika anawaka kama umeme hakuna aliyethubutu kumwangalia, jiwe lilimkimbia likatoka kaburini, walinzi walizimia kwa mwako wa nuru yake hawakuweza kumzuia Yesu tena asifufuke, ndivyo anavyofanya kwako leo, waliokushikilia wataachia, waliokalia Baraka zao wataziachia wenyewe maana hawatavumilia huo moto, waliokuonea watakukimbia, nchi na misingi ya gereza inafunguka, vifungo vyote vinakuachia kwa jina la Yesu.

2Wafalme 3:26 “Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.” Mfalme akaona amtoe mwanawe mkubwa sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta, na maandiko yanasema ikatokea hasiraya Bwana juu ya Israel, yaani alitoa kafara ya kiwango cha juu na adui zake Israel wakatawanyika.
Kadharika kwako

waganga na wachawi wakiona unawashinda kwenye ulimwengu wa roho na wanatoa kafara ili kupata nguvu kubwa zaidi za kuwatawanya na kuwafarakanishwa.
Kwako leo kafara zao hazitafanikiwa, mipango yao waliyoipanga juu yako haitakuwa. Kwa damu ya mwanakondoo wewe ni mshindi, mauti iliyoelekezwa kwako haitakupata, uchawi walinaochawia maisha yako na biashara yako hayatakuwa, utastawi kwa jina la Yesu, utainuka kwa jina la Yesu na utawashinda kwa damu ya mwanakondoo. Damu ya mwanakondoo ndiyo kafara bora kuliko zote na kwa hiyo tunawashainda wote wasimamao kinyume chetu na kwa hayo tunawapiga wote watesao maisha yetu na kila chanzo cha tatizo lako likome kwa Damu ya Yesu Kristo wa Nazareth.
Amen
Watu waliojitokeza kumpa Yesu maisha yao baada ya mahubiri

0 comments:

Post a Comment

Prayers (Andika Maombi yako Hapa)

Name

Email *

Message *

Sponsor

Kama unapenda kuchangia Huduma Yetu Tafadhali wasiliana nasi