GLORY OF CHRIST

Genesis 1:28. God blessed them and said to them, “Be fruitful and increase in number; fill the earth and subdue it. Rule over the fish in the sea and the birds in the sky and over every living creature that moves on the ground..

Wednesday, July 16, 2014

VIKAO VYA UHARIBIFU



SOMO: VIKAO VYA UHARIBIFU. Tarehe 13  July 2014


RP Adriano akihubiri
Na. RP Adriano


Duniani kote jambo lolote linapotakiwa kufanyika, vikao hukaliwa. Mfano katiba yetu ililazimu wateuliwe wajumbe ili kujadili juu ya utekelezaji wa mchakato wake, na hata katika ulimwengu wa roho, mambo yanafanyika kwa vikao mbalimbali vya uharibifu kukaa.


2Nyakati18:15-21, 1Wafalme16:29-34, 1Wafalme 21:17-21.


“Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe, usiniambie neno ila yaliyo kweli, kwa jina la Bwana? Akasema, Naliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji; Bwana akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani. Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Je! Sikukuambia, hatanibashiria mema, ila mabaya? Mikaya akasema, Sikieni basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi na jeshi lote la mbinguni wamesimama mkono wake wa kuume na wa kushoto. Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu mfalme wa Israeli, ili akwee Ramoth-gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka, ukafanye hivyo.”



Israel walipokuwa wanaingia Yeriko walikutana na kivuizi cha ukuta na Bwana Mungu akamwambia Yoshua muuzunguke mara saba, na baada ya kufanya hivyo Bwana akawapa ushindi. Inawezekana watu wa yeriko walipowaona wakizunguka waliwacheka bali wao walimwamini Bwana, na ndivyo ilivyo kwako yumkini watu hawakuelewi nini unachokiamini au unachokifanya, lakini ipo Imani katika Mungu, upo kanisani kuyasikiliza maelekezo ya Mungu  na Mungu ndiye atupaye nguvu ya kuharibu vikao vyote vya uharibifu, nguvu ya kutoka kwenye kila gereza na vifungo vya kishetani leo iwe ushindi wako na uhuru wako. Katika Bwana tunazo nguvu zitakazo angusha mipango yote ya kishetani juu yako, wanaopanga kuua biashara wataangushwa kama Yeriko, wanaoharibu watoto wako, biashara yako nk waangushwe chini kwa jina la Yesu Kristo aliye hai..


Mtu mwovu hawezi kutamalaki bila kuua mtu, Ahabu na mkewe Yezebeli walimuua Naboth ili wamiliki shamba lake na haya ni madhara yaliyotokea kwa ahabu baada ya kumuoa Yezebeli mwabudu mungu baali. Yezebeli aliweka kikao cha kumdhuru Naboth na hata kwako kuna vikao vinakaliwa na wabaya wako ili kuharibu mambo yako lakini katika jina la Yesu HAYATAKUWA wanayoyapanga, hawatafanikiwa juu ya mipango yao yenye hila dhidi yako katika jina la Yesu.


SNP Mwangasa wa pili kulia, AP Hosea wa pili kushoto na wachungaji wengine wakisikiliza neno.
Nina HABARI NJEMA KWAKO kwamba “kila hila na kila mtego na aliyetega mitego, vikao na wajumbe wa vikao vyenye kukusudia mabaya juu yako, kila hasara na aliyeileta, mateso na mwenye kuyaleta katika Jina la Yesu Kristo nayarudisha kwao wenyewe, kila mateso na aliyeyaleta, magonjwa na mwenye kuyaleta naamuru kwa Jina la Yesu sasa yatoke na kuwaacha huru watu wa Mungu. Nawashamburia wote walioko mapolini na kuzimu na mahali popote walipkusanyanyika kinyume chako wasambaratike, vikao vyao viharibiwe na tunawafyeka na kupaharibu mahali pao. Mawakala wote wa sheteni awe ndugu au mtu baki asababishaye mateso juu ya maisha yako ahabiwe mwenyewe. na ubakie mtu huru na aliyefanikiwa kwa DAMU YA MWANAKONDOO” Ameni.

RP Adrian akihudumia watu kuwafungua katika vifungo mbalimbali.

RP Adrian akiwaita watu kumpa Yesu maisha yao.

Baba huyu akipita mbele kumpa Yesu maisha yake kwa namna ya kusarenda kabisa

Watu waliopita mbele kumpa Yesu maisha yao wakipwa maelekezo

Watu wakiombewa baada ya neno na kufunguliwa kutoka kwenye vifungo mbalimbali








0 comments:

Post a Comment

Prayers (Andika Maombi yako Hapa)

Name

Email *

Message *

Sponsor

Kama unapenda kuchangia Huduma Yetu Tafadhali wasiliana nasi