JE, MUOTA NDOTO ANAWEZA KUFA KABLA YA NDOTO YAKE KUTIMIA? Na AP
Hosea Shaban
Tarehe : 13-Mar-2014
AP Hosea Shaban |
Mwanzo->45:1-9
Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote
waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele
yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. Akapaza
sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao
wakasikia.
Majeshi ya bwana wakisiliza neno |
Yusufu akawaambia ndugu
zake, “Mimi ndimi Yusufu; baba yangu
angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu
mbele yake.
Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia.
Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri.
Basi sasa, msihuzunike, wala msihudhike nafsi zenu, kwa kuniuza
huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. Maana miaka
hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima
wala kuvuna.
Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na
kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu. Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu;
naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na
mtawala katika nchi yote ya Misri.
Fanyeni haraka, mmwendee baba yangu, mkamwambie, Hivi ndivyo
asemavyo mwanao Yusufu, Mungu ameniweka kuwa bwana katika Misri yote, basi
unishukie, usikawie.”
AP Hosea akimwombea huyu mama |
Kila mtu anayo ndoto kwa
habari ya maisha yake. Lakini wapo wajanja wa mjini ambao ni wajumbe/watumishi
wa shetani huku duniani wenye uwezo wa kufunika ndoto ya mtu. Pia ni muhimu kufahamu
ya kwamba humu duniani kuna watu wasiofaa kwenye maisha ya mtu.
Tunaona ya kuwa ndugu zake
Yusuph walimtenda mabaya ili wamwuangamize, lakini ashukuriwe Mungu nduguze na Yusuph walikuwa daraja la yeye
kupanda juu kupitia nyota yake.
Yamkini umekuja leo kwenye
nyumba ya Ufufuo na Uzima na umeshindwa kupiga hatua kwa sababu ya ndugu, mchumba,
mume au mke amekuacha wala usiwe na wasi wasi kwa maana inakuja siku ambayo
Mungu atasababisha ndoto yako itimie kwa namna yeyote,
Hatma na ndoto za mtu huyu zikirudishwa |
Tena usiogope kwa maana
lile jaribu au pito unalopitia ni la muda tu kwa sababu hakika halitakuangamiza
na ni Mungu ameruhusu usiangamie ili
adui/watesi wako washuhudie na kuliona lile jambo jipya litakalotokea kwa maana
historia ya maisha yako itabadilika.
Ni kweli yawezekana sasa
hivi watu wanakudharau kulingana na hali ngumu ya maisha unayopitia, Ila
usiogope kwa maana lipo jambo ambalo Mungu atalifanya maishani mwako
litakalowasababishia adui na watesi wako wanapenda au wasipende!!!
Historia ya maisha yako ni
lazima itabadilika acha waendelee kijivuna wanachojivunia ila wewe mkamate Yesu
Kristo pekee ili ujivunie yeye.
Hatma na ndoto za mama huyu zikirudishwa |
Pia tunaona mfano mzuri
kwenye biblia wa Gidioni alikuwa anajiona ya kuwa hafai kama wewe
unavyojidharau na kujiona ya kuwa haufai. Mungu anasema unafaa. Nakutangazia
hautakufa kabla ndoto zako kutimia katika jina la Yesu Kristo wa nazaret.
0 comments:
Post a Comment