GLORY OF CHRIST

Genesis 1:28. God blessed them and said to them, “Be fruitful and increase in number; fill the earth and subdue it. Rule over the fish in the sea and the birds in the sky and over every living creature that moves on the ground..

Saturday, March 15, 2014

NI MKESHA MKUBWA NDANI YA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA (MOSHI)


NI  MKESHA MKUBWA  NDANI YA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA (MOSHI)
            Na Snp King Mwangasa  ijumaa tar 15/march/2014
Snp King Mwangasa
 Matendo ya mitume->16:25-26
Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.”


Paulo na Sila walikamatwa kwa kosa la kumtoa mapepo binti aliyekuwa na pepo wa utambuzi,Wakashangaa kuona wanakamatwa na viongozi wote wa mji ule,Biblia inasema wakakokotwa mpaka sokoni wakavuliwa nguo na kupigwa saana!

          KUNA MAMBO YA KUJIFUNZA HAPA!
1/Jambo la kuvuliwa nguo ni  la aibu saana kwa mtu kama Paulo mwanasheria msomi mashuhuri katika Israeli.

2/Walipigwa saana kwa kosa tu la kumtumikia Mungu jambo ambalo usingetarajia kuwa ndiyo sababu ya kipigo,waliletwa gerezani wakiwa katika hali ya maumivu makali

3/Walikuwa gerezani huku wakiwa wanakumbuka jinsi walivyo aibishwa kwa kuvuliwa nguo  tena walikuwa chumba cha ndani huku wakiwa wamefungwa,Hayo yote ni maumivu makali katika hali ya kibinadamu

4/Paulo na Sila walikuwa na kila sababu kumlaumu Mungu kwa kuwatosa bila msaada huku wamepata tatizo wakiwa katika kazi ya kumtumikia Mungu.

5/Inawezekana walimtarajia Bwana awatoe saa 12 jioni,saa 1usiku,saa3,usiku mpaka ikafika saa 7 usiku bado wanashangaa hakuna mtu yeyote aliyejitokeza kuwasaidia,Katika hali ya kawaida ungetarajia Paulo na Sila kuwa wamekata tama lakini kinyume chake Biblia inasema panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kumuimbia Mungu nyimbo za sifa,Ni jambo ambalo lilipelekea hata wafungwa wengine kuwashangaa

6/Mungu aliposikia sauti za nyimbo za kumsifu yeye,Akashangaa  kusikia sauti zile zinatokea gerezani ndipo hasira ya Mungu ikawaka kukatokea tetemeko kuu la nchi,misingi ya gereza ikatikisika na milango ya gereza ikafunguka  na vifungo vikawafunguka wafungwa wote gerezani




Majeshi ya Bwana yakiwa makini kumsikiliza Daddy!

Ndugu zangu yawezekana uko kwenye maumivu ya ugonjwa,Naomba nikutie moyo kuwa hata Paulo na Sila walikuwa kwenye maumivu makali lakini wakayadharau na kumwimbia Mungu hata katikati ya maumivu ,Pia yawezekana uko katika mapito magumu,mambo yamesonga,balaa zimekuandama na ndani yako kuna kelele nyingi za kukuvunja moyo umekosa msaada kabisa hakuna hata mtu mmoja anayeonyesha nia ya kukusaidia,Tambua huo ni usiku wa manane kwakoàNakusihi katika jina la Yesu Kristo zungumza upya na nafsi yako na Uiambie akili yako kwamba imebaki nafasi ya Yesu tu!


Ungana nasi katika mkesha huu wenye uwepo wa Ajabu embu anza kumwimbia Bwana nyimbo za kusifu na kuabudu huku ukimwambia umebaki wewe peke yako.Mwambie Yesu hata katika tabu hii nakungoja wewe tu!

Kama ambavyo gereza la Paulo na Sila lilivyotokewa na tetemelo la ghafla ndivyo na Bwana atakavyokutendea wewe  muujiza wa ghafla
Pokea muujiza wa uponyaji wa ghafla kwa jina la Yesu Kristo.
Pokea muujiza wa Baraka wa ghafla kwa jina la Yesu  Kristo.
Pkea muujiza wa kufunguliwa wa ghafla kwa jina la Yesu Kristo

0 comments:

Post a Comment

Prayers (Andika Maombi yako Hapa)

Name

Email *

Message *

Sponsor

Kama unapenda kuchangia Huduma Yetu Tafadhali wasiliana nasi