SAA YA UFUFUO NA UZIMA (MOSHI)
Somo:KUMBE HAIKUWA KWELI - Na Ap Hosea
AP Hosea |
Watu wengi leo duniani wamekuwa wakiteswa na taarifa walizozipokea maishani mwao.
Kulikuwa na familia ya mzee Yakobo,Yakobo alikuwa na watoto wakike na wakiume lakini mtoto wake mmoja aitwaye Yusuphu aliyempata uzeeni,Na Yusuphu huyu alipokuwa na miaka 17 Biblia inaelezea kuwa alipata kibali,upendeleo machoni pa babaye na tunaona wazi ya kuwa sababu ya yeye kupendwa na baba yake iliwasababishia nduguze wote wamchukie,kwa sababu waliona Yusuphu anapendwa kuliko wao ikaanza kuinuka chuki ndani yao,wakaanza kumchukia Yusuphu na hawakuongea naye kwa amani kwa maana mazungumzo yao waliokuwa wanazungumza kinyume na mdogo wao hayakuwa ya amani,Biblia inaendelea kuelezea kwamba Yusuphu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia na ndoto hiyo alikuwa Yusuphu na ndugu zake naye akawaelezea akisema"sikieni ndoto hii niliyoiota.
Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu."Laikini nduguze Yusuphu hawakumuelewa kabisa,Kwa maana walimwambia"Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.
Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.
Daddy King Mwangasa Akifuta taarifa mbaya |
Ap Hosea akifuta taarifa mbaya |
Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali.Jambo la ajabu kabisa ambalo ndugu zake walilifanya kwa Yusuph,Waliichukuwa Kanzu yake na wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika damu.
Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo.
Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa.Baba alipoletewa taarifa hizi
Aliyararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi.
Hapa tunaona ya kuwa Yusuphu hakuwa amekufa bali yeye alikuwa ameuzwa tu,Sasa leo tunaenda kuzifuta kila aina ya taarifa zisizo na ukweli maishani mwetu kwa Damu ya Mwanakondoo, Yawezekana wewe unayesoma hizi habari njema sasa hivi,Umeshindwa kupata mtoto kwa sababu mfuko wako wa uzazi umeharibika,na jinsi madaktari walivyokuwa wataalamu baada ya vipimo wanakupa jibu ambalo actually limebeba taarifa mbaya, Wakati huu ndugu msomaji haijalishi upo kwenye hali gani unayopitia kimaisha cha msingi ni kubadilisha taarifa mbaya zote ambazo ufahamu wako ulishakubali kuzisajili katika akili yako na kuzigeuza kuwa taarifa njema kwa DAMU YA YESU KRISTO!!!
0 comments:
Post a Comment