Nabii mke Rachel, kutokea kabila la Yudah nchini Israel, amekuwepo katika ardhi ya Tanzania mjini Moshi, kilimanjaro kinabii, akiwa ametumwa na Mungu kwa makusudi makuu.
Kuondoa giza lililokuwa limetanda anga lote la paa la Afrika yaani kilimanjaro ambalo limekuwa likiifunika Afrika kwa ujumla. (Kumbuka unapozungumzia kilimanjaro ndipo mahali pa juu pa Afrika yote.)
Kunyamazisha kila damu za wanadamu na wanyama zilizokuwa zikipiga kelele kutokana na makafara yaliyokuwa yakifanywa miaka nenda rudi ndani ya nchi hii, ibada za sanamu zilizofanyika na si tu zimefanywa na watu wa kilimanjaro, hasha na wageni kutoka nje ya nchi wanaoupanda mlima wamekuwa wakifanya matambiko juu ya mlima huu.
Kuwaunganisha Africa yote na Baraka za baba wa Imani Ibrahim kupititia taifa takatifu la Israel ukianzia na kilimanja.
Sambamba na hayo limetendeka tukio la kihistoria la Toba ya kweli kwa kuorodhesha makosa, hatia na dhambi zote zikachomwa moto na kutuacha huru.
Ametujulisha juu ya wokovu tulionao kwamba ni kwa neema tu, tumeupata na kwa gharama ya wayahudi kutoupata kwanza; na kwa kutopokea wao kwanza kulilenga kutufanya sisi tuupate kwanza ndipo wao wafuate. Kwa sababu hiyo kila aliyepokea neema hii analo jukumu la kuomba kwa ajili ya Israel ili waikubali neema hii ya wokovu kupia Yeshua Amashia (Yesu Masia)
0 comments:
Post a Comment