NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA (MOSHI) 19tar03/2014
Somo:TENA NASEMA FURAHINI
Na Ap HOSEA
Ap Hosea katika Ibada |
Wafilipi->4:4-7
“ Furahini katika Bwana
sikuzote; tena nasema, Furahini.
Upole wenu na ujulikane na watu
wote. Bwana yu karibu.
Msijisumbue
kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa
kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Na amani ya Mungu, ipitayo akili
zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”
*Watu wengi leo duniani
hawana amani wala Furaha kwa sababu ya mambo fulani Fulani yaliyojitokeza
maishani mwao yamkini wewe unayesoma maneno haya ya uzima ni mmojawapo kati ya
hawo walio koseshwa furaha,Ahimidiwe Bwana wa majeshi kwa maana yeye ndiye Furaha
ya maisha yetu!
SABABU CHACHE KWA NINI TUFURAHI KATIKA BWANA
1/Tunafurahi katika Bwana tukijua katika Bwana
Imo furaha na amani ya kudumu.
2/Tunafurahi katika Bwana kwa maana ukimpokea
Bwana Yesu nguvu za giza hazina
uwezo juu ya maisha yako tena!
3/Tunafurahi katika Bwana kwa maana kuna
mataifa wanategemea kuona vitu kutoka
kwetu,Ambavyo vitabadilisha mtazamo wa maisha yao!
Majeshi ya Bwana yakishagilia pindi yalipotambuwa Furaha ya kweli ni Yesu pekee. |
*Maandiko yanasema Upole wenu na ujulikane na
watu wote kwa maana Bwana yu karibu ni lazima upole wetu ujulikane na watu wote
ili watu wapate kujifunza kutoka kwetu .
*Tatizo la watu wengi wanapoumizwa na kukoseshwa
amani na furaha,huwa wanaangaika na kutafuta msaada wa kutatua matatizo yao kwa wanadamu,Bali leo Eeh mtu wa
Mungu nakusihi kwa jina la YESU KRISTO chukuwa hatua ya kumgeukia Mungu na kuamini ya
kuwa yeye ndiye njia pekee ya kutatua matatizo yaliyokukosesha furaha maishani
mwako.
*Tunaona hata mtumishi wa Mungu Daudi katika
shida yake hakuwaita wanadamu,Bali
alitambuwa msaada wake unapatikana kwa Bwana YESU pekee,Naye akageuza
mtazamo wake kutoka kwa wanadamu na akachukua hatua ya kumuamini Mungu pekee
kwa Imani yake yote,Ni maombi yangu mbele za uso wa Mungu jioni ya leo uchukuwe
hatua ya kuondoa tegemeo lako kwa wanadamu na kuliamishia kwa Mungu kwa maana
Imeandikwa “Amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu na moyoni mwake amemuacha
Bwana.
*Yakupasa kufahamu kuwa unapoingia kwenye
matatizo au shida mbali mbali zitakazoweza kuitowesha furaha ya Mungu maishani
mwako ni lazima ujifunze akilini mwako
wa kumuendea ni nani? Na ni jambo jema tena lafaa kama nini! kupeleka haja za mioyo yetu kwa Bwana Yesu!
Pia ni lazima ufahamu ya kuwa umembeba nani! Ndani ya moyo wako kwa sababu kuna
baadhi ya watu wamekuwa wakipita katika vipindi vigumu maishani mwao kwa sababu
hawajajua waliye naye ni Mkuu kuliko mkuu wa Ulimwengu huu!
Makamanda wa Bwana Yesu wakimsihi Bwana Yesu kuwa furaha pekee ya maisha yao |