Na SNP King Mwangasa.
Ni rahisi mtu kujiuliza
kurudisha nyota tena? Kulikoni mpaka kurudisha nyota?
Unajua nyota kwenye
biblia inamaanisha kipawa cha mtu au inawakilisha kipawa cha mtu ambacho ndiyo
dira na mwelekeo wa maisha ya mtu. Katika ulimwengu wa roho kila mtu ana
kiashilia kinachoonyesha maisha yake na kiashilia hicho ndicho huitwa nyota. Kila
mtu aliyezaliwa, amezaliwa kwa kusudi na hata kama njia iliyotumika kumleta
duniani mtu huyo tunaiona si sahihi machoni petu lakini bado Mungu aliruhusu
njia hiyo kumleta mtu maalumu duniani ili atimize kusudi lake.
|
SNP King Mwangasa akifundisha |
Yusuph alipoota ndoto ya
kwanza kuhusu mganda wake kusimama katikati na ya kaka zake kumwinamia tunaweza
kusema kweli hapa wivu una sababu kwa nini miganda yak ka zake imwinamie yeye? Na
katika ndoto ya pili anaota nyota 11, jua na mwezi vinamwinamia, matoko a ndoto
hii anachukiwa zaidi na baba anamkemea. Hapa suala si nyota wala mwezi na jua
tuvionavyo angani? Ukali huu wa baba(Yakobo mtumishi wa Mungu, Yule aliyesema
na Mungu baada ya kutia mafuta kule Betheli, aliye baba wa Israel wote) na
chuki za ndugu zake ni kuhusu uelekeo wa maisha yao, kipawa. Yakobo aliyajua
haya, alipata tafsri sahihi na ndo maana akayahifadhi.
Mathayo 2:1-10.
Walitoka mamajusi(wajuzi
wa nyota) wa mashariki wakafika mpaka ikulu na kumuuliza “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana
tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia” Jambo la ajabu
sana kwamba Yesu ambaye ni baba yetu, ni jina halisi la Mungu, mwokozi wetu, Eti
alipozaliwa kuna kitu kilichotambulisha kuzaliwa kwake, hata hawa wachawi(Magi
au Astrologers ) wakaona tokea mashariki ya mbali yaani watu tokea china au Thailand
pengine au Japan nyota ya Yesu kabla hata hajazaliwa wakasafiri kwa ngalawa za
kusukumwa na upepo pengine kutokana na tekinolojia ya wakati huo mpaka wakafika
Yerusalemu kwa wakati. Haiishii hapo wamemkuta mfalme Herode badala ya
kumsujudia yeye bado wanauliza habari za katoto kalikozaliwa na wanadiriki
kusema wanataka kumsujudia. (Kinachowalazimisha kusujudu ni Nyota) Hawa si
wajinga, ni wataalam hawa katika ulimwengu wa roho wanajua wanachokifanya.
Kumbe kama Yesu
alipozaliwa alikuwa na nyota yake, vivyo kila aliyezaliwa ana nyota yake.
Kwa nini basi hawa
mamajusi wa mashariki waende kumsujudia mtoto tu? Mfalme Herode alikuwepo hapo,
haikutosha kumsujudu yeye? isitoshe huko walikotokea kuna wafalme pia kwa nini
wasiwasujudie hao na kuridhika kama suala lilikuwa ni kuwasujudia wafalme? Jibu
ni hili, kwa kawaida wachawi, wanga, wasomanyota na watu wote wa giza hupata
nguvu kwa shetani ambaye ni kiongozi mkuu wa falme zote na mamlaza za giza.
Kuzaliwa kwa Yesu Kristo, nuru iliangaza ulimwenguni mwote, giza likakosa nguvu(Yoh1:4b-5),
kulitikisa kila falme zote na kusababisha taharuki katika ufalme wa shetani.
Watu hawa walitafuta ni nini kimepelekea kukosa nguvu, wakajua kuna mfalme wa
wayahudi amezaliwa na alishanenwa katika ulimwengu wa roho, ana uweza na nguvu
za kushinda miliki zote na kwa kuwa wachawi ni watu wa rohoni kwa upande wa
giza, wakatafsiri na kujua hayo.
Watu wa rohoni upande wa
shetan (Wachawi) wanaweza kuiona nyota
ya mtu tangu siku anapozaliwa. Wakiiona nyota wanajua nyota inawakilisha kipawa
cha mtu.
KAZI
ZA NYOTA/KIPAWA CHA MTU
1.Hufanya
mtu kuwa mahiri katika utendaji (Effectiveness)
2.Humfanya
mtu kuwa mbunifu(Creative)
3.Kipawa
humsaidia mtu kutenda kwa ufanisi (Efficiency)
4.Nyota
au kipawa huleta mvuto, watu huvutiwa na wewe (attraction)
5.
Inasababisha mtu akubalike kupata kibali
(Divine Acceptance/fever )
6.
Kinamfanya mtu awe jasiri ujasiri wa
kile, humpa mtu ujasiri wa jambo analolifanya (Divine Boldness)
Niishie kwa hayo
machache, kwamba nyota ya mtu inapokuwa iko pamoja na yeye, na ikiwa nyota ya
mtu imefunikwa inasababisha mambo hayo yasitendeke juu yako.
Mungu alivyotuumba
anataka tuwe na ufanisi, umahiri, ubunifu, kibali, ujasiri na mvuto katika
kutenda.
Shetani yeye kumbuka ni kerubi afunikaye
(Ezekiel 28:14) na hata sasa anatumia hila zake kufunika mema ya watu. Kuna
matatizo yanaanzia siku mtu anapozaliwa kwa maelekezo na hila za shetani. Wapo
waliofunikwa nyota zao na wazalisha kama yule mzalishaji wa Peresi na Zera na
wengine waliacha hai. (Mwanzo
38:27-30, 1 Nyakati 27:2,3 Nehemia 11:6, Kutoka 1:15-17)
Zera maisha yake yalitokana na kitu alichokifanya mzalishaji wao, wengine walioachwa
hai pamoja na vipawa vyao kama wazalisha wa waebrania waliogoma kutekeleza amri
ya farao na hatimaye wakawahifadhi hai pamoja na Vipawa vyao. Pia mavazi ya
kwanza kazivaa au zawadi unazopewa vyaweza tumika kufunika maisha ya mtu. Siku
mtu anapozaliwa anaweza kufunikwa nyota ya maisha yake, maana uhai unaanzia
siku mimba inapotungwa na maisha ya mtu yanaanzia siku anapozaliwa na katika
mda anapokuwa humo tumboni anakuwa salama, lakini siku unazaliwa mlinzi
aliyekuwa akikulinda tumboni placenta (kondo) hubakia kwa mzalisha. Mzalisha
anaweza kumtumia huyo mlinzi katika ulimwengu wa roho na kuyaharibu maisha ya
mtu.
Ezekiel 16:4,5.
Ezekiel anawatabiri
Israel siku alipozaliwa na katika kukua kwake. Shetani anawinda maisha ya mtu
tangu day one. Shetani anafunika kipawa hukohuko rohoni kwa kuwa nyota au
kipawa hakiko mwilini. Na mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba iitwayo mwili.
Roho ndiyo mmliki wa kipawa na inatumia mwili kudhihirisha kipawa, hivyo
shetani anafunika rohoni ili kisijidhihirike katika mwili.
Isaya 47:12-15.
Wachawi, waganga na
wasomanyota wanashirikiana kufunika nyota na wanaweza kuharibu maisha ya mtu.
Faraki ni elimu ya uchawi. Watu awa aina hii wote ni mtandao wa shetani.
Mhubiri 9:11
…. si wenye
mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si
wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye
ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Ukifunikwa
nyota yako wakatia wa bahati yako ukifika wanapewa wengine.
Isay 42:22
Chukua hatua
sasa tuombe pamoja kwa mamlaka, tumwambie shetani toka na uachie nyota yangu,
maisha yangu yachanue tena maana kwa kusudi hili mwana wa adamu alidhihirishwa
ili azivunje kazi ibirisi, naye ndiye nuru ya watu na nuru yake yang’aa gizani wala
giza halikuiweza, nawe hira zote za giza zisikuweze, kitu cha thamani
alichokuumbia Mungu kionekne kwako katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
|
Mamia ya watu wakisikiliza ujumbe wakati alipokuwa akihubiri SNP King Mwangasa |
|
Platform Ministry wakiongoza mamia ya watu kwenye ibada yasifa na kuabudu |
|
Wakati wa maombezi |