GLORY OF CHRIST

Genesis 1:28. God blessed them and said to them, “Be fruitful and increase in number; fill the earth and subdue it. Rule over the fish in the sea and the birds in the sky and over every living creature that moves on the ground..

Waumini wa Kanisa la Ufufuo Na Uzima Moshi

Kutoka->14:13-14 (Kutoka Katika Nchi ya Utumwa Na Snp. Mwangasa)

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa La Ufufuo na Uzima Moshi

Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima

MAJESHI,MAJESHI, MAJESHI YA BWANA

Sunday, April 24, 2016

MAOMBI YA KURUDISHA NYOTA ILIYOFUNIKWA

Na SNP King Mwangasa.                                                                         
Ni rahisi mtu kujiuliza kurudisha nyota tena? Kulikoni mpaka kurudisha nyota?
Unajua nyota kwenye biblia inamaanisha kipawa cha mtu au inawakilisha kipawa cha mtu ambacho ndiyo dira na mwelekeo wa maisha ya mtu. Katika ulimwengu wa roho kila mtu ana kiashilia kinachoonyesha maisha yake na kiashilia hicho ndicho huitwa nyota. Kila mtu aliyezaliwa, amezaliwa kwa kusudi na hata kama njia iliyotumika kumleta duniani mtu huyo tunaiona si sahihi machoni petu lakini bado Mungu aliruhusu njia hiyo kumleta mtu maalumu duniani ili atimize kusudi lake.

SNP King Mwangasa akifundisha
 Mwanzo 37:5-
Yusuph alipoota ndoto ya kwanza kuhusu mganda wake kusimama katikati na ya kaka zake kumwinamia tunaweza kusema kweli hapa wivu una sababu kwa nini miganda yak ka zake imwinamie yeye? Na katika ndoto ya pili anaota nyota 11, jua na mwezi vinamwinamia, matoko a ndoto hii anachukiwa zaidi na baba anamkemea. Hapa suala si nyota wala mwezi na jua tuvionavyo angani? Ukali huu wa baba(Yakobo mtumishi wa Mungu, Yule aliyesema na Mungu baada ya kutia mafuta kule Betheli, aliye baba wa Israel wote) na chuki za ndugu zake ni kuhusu uelekeo wa maisha yao, kipawa. Yakobo aliyajua haya, alipata tafsri sahihi na ndo maana akayahifadhi.

Mathayo 2:1-10.
Walitoka mamajusi(wajuzi wa nyota) wa mashariki wakafika mpaka ikulu na kumuuliza “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia” Jambo la ajabu sana kwamba Yesu ambaye ni baba yetu, ni jina halisi la Mungu, mwokozi wetu, Eti alipozaliwa kuna kitu kilichotambulisha kuzaliwa kwake, hata hawa wachawi(Magi au Astrologers ) wakaona tokea mashariki ya mbali yaani watu tokea china au Thailand pengine au Japan nyota ya Yesu kabla hata hajazaliwa wakasafiri kwa ngalawa za kusukumwa na upepo pengine kutokana na tekinolojia ya wakati huo mpaka wakafika Yerusalemu kwa wakati. Haiishii hapo wamemkuta mfalme Herode badala ya kumsujudia yeye bado wanauliza habari za katoto kalikozaliwa na wanadiriki kusema wanataka kumsujudia. (Kinachowalazimisha kusujudu ni Nyota) Hawa si wajinga, ni wataalam hawa katika ulimwengu wa roho wanajua wanachokifanya.

Kumbe kama Yesu alipozaliwa alikuwa na nyota yake, vivyo kila aliyezaliwa ana nyota yake.
Kwa nini basi hawa mamajusi wa mashariki waende kumsujudia mtoto tu? Mfalme Herode alikuwepo hapo, haikutosha kumsujudu yeye? isitoshe huko walikotokea kuna wafalme pia kwa nini wasiwasujudie hao na kuridhika kama suala lilikuwa ni kuwasujudia wafalme? Jibu ni hili, kwa kawaida wachawi, wanga, wasomanyota na watu wote wa giza hupata nguvu kwa shetani ambaye ni kiongozi mkuu wa falme zote na mamlaza za giza. Kuzaliwa kwa Yesu Kristo, nuru iliangaza ulimwenguni mwote, giza likakosa nguvu(Yoh1:4b-5), kulitikisa kila falme zote na kusababisha taharuki katika ufalme wa shetani. Watu hawa walitafuta ni nini kimepelekea kukosa nguvu, wakajua kuna mfalme wa wayahudi amezaliwa na alishanenwa katika ulimwengu wa roho, ana uweza na nguvu za kushinda miliki zote na kwa kuwa wachawi ni watu wa rohoni kwa upande wa giza, wakatafsiri na kujua hayo.

Watu wa rohoni upande wa shetan (Wachawi)  wanaweza kuiona nyota ya mtu tangu siku anapozaliwa. Wakiiona nyota wanajua nyota inawakilisha kipawa cha mtu.

KAZI ZA NYOTA/KIPAWA CHA MTU
1.Hufanya mtu kuwa mahiri katika utendaji (Effectiveness)
2.Humfanya mtu kuwa mbunifu(Creative) 
3.Kipawa humsaidia mtu kutenda kwa ufanisi (Efficiency)
4.Nyota au kipawa huleta mvuto, watu huvutiwa na wewe (attraction)
5. Inasababisha mtu akubalike  kupata kibali (Divine Acceptance/fever )
6. Kinamfanya mtu awe jasiri  ujasiri wa kile, humpa mtu ujasiri wa jambo analolifanya (Divine Boldness)

Niishie kwa hayo machache, kwamba nyota ya mtu inapokuwa iko pamoja na yeye, na ikiwa nyota ya mtu imefunikwa inasababisha mambo hayo yasitendeke juu yako.
Mungu alivyotuumba anataka tuwe na ufanisi, umahiri, ubunifu, kibali, ujasiri na mvuto katika kutenda.

 Shetani yeye kumbuka ni kerubi afunikaye (Ezekiel 28:14) na hata sasa anatumia hila zake kufunika mema ya watu. Kuna matatizo yanaanzia siku mtu anapozaliwa kwa maelekezo na hila za shetani. Wapo waliofunikwa nyota zao na wazalisha kama yule mzalishaji wa Peresi na Zera na wengine waliacha hai. (Mwanzo 38:27-30, 1 Nyakati 27:2,3 Nehemia 11:6, Kutoka 1:15-17) Zera maisha yake yalitokana na kitu alichokifanya mzalishaji wao, wengine walioachwa hai pamoja na vipawa vyao kama wazalisha wa waebrania waliogoma kutekeleza amri ya farao na hatimaye wakawahifadhi hai pamoja na Vipawa vyao. Pia mavazi ya kwanza kazivaa au zawadi unazopewa vyaweza tumika kufunika maisha ya mtu. Siku mtu anapozaliwa anaweza kufunikwa nyota ya maisha yake, maana uhai unaanzia siku mimba inapotungwa na maisha ya mtu yanaanzia siku anapozaliwa na katika mda anapokuwa humo tumboni anakuwa salama, lakini siku unazaliwa mlinzi aliyekuwa akikulinda tumboni placenta (kondo) hubakia kwa mzalisha. Mzalisha anaweza kumtumia huyo mlinzi katika ulimwengu wa roho na kuyaharibu maisha ya mtu.

Ezekiel 16:4,5.
Ezekiel anawatabiri Israel siku alipozaliwa na katika kukua kwake. Shetani anawinda maisha ya mtu tangu day one. Shetani anafunika kipawa hukohuko rohoni kwa kuwa nyota au kipawa hakiko mwilini. Na mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba iitwayo mwili. Roho ndiyo mmliki wa kipawa na inatumia mwili kudhihirisha kipawa, hivyo shetani anafunika rohoni ili kisijidhihirike katika mwili.

Isaya 47:12-15.
Wachawi, waganga na wasomanyota wanashirikiana kufunika nyota na wanaweza kuharibu maisha ya mtu. Faraki ni elimu ya uchawi. Watu awa aina hii wote ni mtandao wa shetani.

Mhubiri 9:11
…. si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Ukifunikwa nyota yako wakatia wa bahati yako ukifika wanapewa wengine.

Isay 42:22

Chukua hatua sasa tuombe pamoja kwa mamlaka, tumwambie shetani toka na uachie nyota yangu, maisha yangu yachanue tena maana kwa kusudi hili mwana wa adamu alidhihirishwa ili azivunje kazi ibirisi, naye ndiye nuru ya watu na nuru yake yang’aa gizani wala giza halikuiweza, nawe hira zote za giza zisikuweze, kitu cha thamani alichokuumbia Mungu kionekne kwako katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Mamia ya watu wakisikiliza ujumbe wakati alipokuwa akihubiri SNP King Mwangasa

Platform Ministry wakiongoza mamia ya watu kwenye ibada yasifa na kuabudu
Wakati wa maombezi

Sunday, April 17, 2016

Matukio ya ibada ya ubatizo ufufuo na uzima moshi kilimanjaro tarehe 02..01.2015

Ibada ya ubatizo ya mamia ya watu ikiongozwa na SNP King Mwangasa  na jopo la wasaidizi wake,ufufuo na uzima kilimanjaro

Ibada ya ubatizo ya mamia ya watu ikiongozwa na SNP King Mwangasa  na jopo la wasaidizi wake,ufufuo na  uzima

 Ibada ya ubatizo ya mamia ya watu ikiongozwa na SNP King Mwangasa  na jopo la wasaidizi wake,ufufuo na 

Sunday, April 10, 2016

MAOMBI YA KUFUTA ALAMA ZA UHARIBIFU ZILIZOWEKWA NA WAZALASHAJI (WAKUNGA)

Na SNP King Mwangasa                   29/11/2015
          Moja ya watu mhimu sana katika kuzaliwa kwa mtu ni wazalisha au wakunga.
SNP King Mwangasa
Kwa wale waliozaliwa vjijini sana pasipo na hospital basi wakunga wa jadi walihusika na kwa waliozaliwa hospitali basi wakunga wa hospitali walihusika.
        Umhimu wa wazalisha hawa unakuja kutokana na kazi hizi Mhimu wanazozifanya wakati mama mjamzito anapofikia hatua ya kumleta mtu duniani. Zifuatazo ni kazi za wazalisha zile ninazozifahamu na naamini wataalam/madaktari wanaweza kutaja zaidi ya hizi kama zipo.

  1. Kumsaidia mama wakati anapojifungua 
  2. Kumpokea mtoto anapozaliwa 
  3. Kumtenganisha mtoto na mama (Kukata kitovu kilichokuwa kikimwezesha mtoto kupokea chakula kutoka kwa mama) 
  4. Kumsafisha mtoto na kumkagua kama yupo vizuri sambamba na kutambua jinsia yake kama ni wa kike au wa kiume. Na hapa mzalisha atahakikisha anatengeneza mazingira ya kumfanya mtoto alie hali ambayo inampa mtoto score au alama fulani na inamaana kubwa sana katika ufahamu wa mtoto. 
  5. Anamfunika mtoto na nguo 
  6. Anamkabidhi mtoto kwa mama au kwa ndugu wa mama kulingana na mazingira yenyewe hasa pale mama anapomzaa mtoto kwa njia ya upasuaaji ni kawaida kwamba atakuwa hajitambui (Unconscious) kiasi cha kumpokea mtoto.

 Je biblia inatambua hatua hizo hapo juu?
Ezekiel 16:4,5 maandiko yanaeleza wazi kuwa mtoto huyu aliyetajwa hapa hakutendewa mojawapo ya mambo hayo sita.

     Mwanzo 38:27-30, Biblia inatuambia mama aliyekuwa na ujauzito, alipokuwa katika kujifungua mzalisha alimfunga mtoto wa kwanza kitambaa chekundu(Alama) mkononi na hatujui alijuaje kama mama huyu atajifungua watoto mapacha maana hata Ultrasound hazikuwepo wakati huo, mimi sijui utalamu alioutumia. “…mtoto mmoja akatoa mkono, mzalisha akautwaa uzi mwekundu akaufunga mkononi mwake, huku akisema, Huyu ametoka kwanza
Mstari ya 29 unaonyesha huyu mtoto alirudisha mkono na kisha ndugu yake akatoka na mzalisha akamuuliza swali “Mbona umepita kwa nguvu wewe? na hakuishia kumuliza swali akamwambia “Mambo ya nguvu na yakuandame” akaitwa Peresi. Baadae yule aliyerudisha mkono na amewekwa alama ya kitambaa chekundu mkononi akatoka na akaitwa Zera.
Mtoto huyu aliyefungwa mkono inaonyesha mambo yake hayakuwa mazuri sana ukilinganisha na Peresi. Majemedari wa Israel wametanjwa kama watoto wa Peresi na zera haonekani popote katika watu wakuu wa Israel. ( 1 Nyakati 27:2,3 Nehemia 11:6) Maandiko haya yanawataja watoto wa Peresi kama maakida.

     Kutoka 1:15-17, Mfalme wa Misri aliongea na wazalisha. Swali kwa nini Mfalme wa Misri aliamua kuongea na wazalisha wa Waebrania? Kabla ya kuwafuata wazalisha alikubaliana na wasimamizi kuwatendea kwa akili, kufanya kazi ngumu ili wasiongezeke lakini HAIKUFUA DAFU, na akaona njia pekee ya kuwamaliza ni wakati wanapozaliwa na mzalisha ni mtu sahihi na ana nguvu ya kuwaacha hai au kuwaua.
Ufunuo 12:1-6. Shetan ndiye aliyeweka wazo hili kwa Farao na hata baadae akaweka ndani ya Herode ili kumuua mtoto Yesu, ndiye yule yule nyoka wa zamani na hata leo anatumia hila zilezile ili awafunge watu kupitia mawakala wake.

     Je, Unajua ni nini kilitokea ulipozaliwa? Kilitokea nini walipozaliwa watoto wako? Wazazi au ndugu na jamaa zako? Kuna wazalisha wengine wamepewa maelekezo na shetani kama Farao mfalme wa Misri alivyowapa maelekezo Pua na Shifra.
Maisha ya watu wengi yamewekewa alama na wazalisha, wametamkiwa maneno (Mazuri au mabaya). Je unajua ulitamkiwa nini au uliwekewa alama gani?
Uliyezaliwa kwa waganga wa jadi walikutamkia nini? na walikuwekea alama gani? Hata wewe uliyezaliwa Hospitalini wazalisha waliokupokea walikuwa na maelekezo ya nini kifanyike juu yako na kutoka kwa nani, Mungu au kwa shetani? Farao alitoa Amri kwa wazalishaji na shetani anaongea na wazalisha, anawapa maelekezo ya wafanye nini na mtoto anayezaliwa.

     Mikono iliyokupokea duniani ilikufunga na nini? na ilimwakilisha nani? Kinywa kilichokupokea duniani kilinena nini? Je walikuhifadhi hai na baraka zako? Au walizifunga? Au waliziua? Nyota yako ilihifadhiwa hai? au ilifunikwa? Au ilichukuliwa? Au ilifichwa?
Wazalisha hawa Pua na Shifla walikuwa wacha Mungu wakawahifadhi hai na vipawa vyao, na baraka zao. Je wazalisha wako walikuhifadhi hai na baraka zako, heshima yako na vipawa vyako? Jihoji mwenyewe! Kama una shaka, huna hakika!

    Simama basi, na ufute kila alama, na maneno ya wazalisha wako, futa kila madhara yaliyotokana na alama ulizofungwa na maneno uliyotamkiwa, dai chocho wanachokishikilia maishani mwako, yafute maneno yao ya laana waliyoyatamka kwako, ifute mikono yao inayoshikilia maisha yako, futa jina lako popote liliporekodiwa kwa ubaya na wazalisha wako, rudisha biashara yako iliyofungwa siku ulipozaliwa, futa aibu uliyowekewa siku ulipozaliwa na jinene baraka za Mungu kwelikweli na ulinzi wa damu ya Yesu inenayo mema ikufunike na vitu vyote, inene mema, itamke kinyume na kila neno baya, isimame kinyume cha kila alama mbaya na maisha yako yachanue na kung’ara kwa sura halisi ya Kimungu. Kwa maombi haya Bwana akutendee katika jina la Yesu Kristo AMEN.
Hapa chini ni picha za mamia ya watu matukio mbalimbali wakati wa ibada.
Add caption

Prayers (Andika Maombi yako Hapa)

Name

Email *

Message *

Sponsor

Kama unapenda kuchangia Huduma Yetu Tafadhali wasiliana nasi