SOMO:TUMAINI KATIKA DHIKI
NA Pst DAVID MWANGI
Mpendwa dunia tunayo ishi imejaa dhiki na uovu, mpaka
unapoangalia mahali unapoweza kujificha unakosa, Lakini na ashukuliwe Mungu wa
uzima ambaye anatuahidi tumaini hata katika mambo hayo.
Watu wengi duniani wanakaa kama watu ambao hawna tumaini ,
kwa sababu hawajui wakimbilie wapi,, Lakini Usiku wa leo niko na habari njama
kwa ajili yako kwa sababu Yesu Kristo mwana wa Mungu yu hai na analo jawabu la
maisha yako
Katika maandiko matakatifu ya Mungu neno lina sema .
AYUBU 14:7 Kwani yako
matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake
hayatakoma.
8 Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na
shina lake kufa katika udongo;
9
Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche
Mungu ana nena na wewe usiku wa leo na
anasema kuna tumaini kwa wale wote ambao wanaona nikama dunia imefika mwisho.
Wana wa Israeli waliteseka sana mikononi mwa
wa Misri, lakini siku moja Mungu alishuka na kuwapa tumaini kwamba anajiandaa
kuwatoa huko kwenye mateso, Na vivyo hivyo SIKU ya leo Bwana ameshuka leo ili
akuokoe.
Ndugu mpendwa niko na habari njema kwako siku
ya leo, kwa maana bwana amenituma nikwambie ya kwamba uwe na subira, kwa maana
yuko njiani akija kukuletea Baraka zako
Kuna uwezekano uli mwendea daktari na alipo
kupima akakwambia uko na H.I.V au CANCER , na zaidi akakwambia haya magonjwa
hayana tiba, LAKINI MIMI niko na habari
njema kwako na hiyo habari ndio hii ya kwamba ISAIAH 53: 5
Inasema, Bali alijeruhiwa kwa makosa
yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Kuna
uwezekano siku ya leo, umefika mwisho katika maisha, unapoangalia mbele na
nyuma hauoni tumaini lolote, lakini nataka nikutie moyo ya kwamba kesho mema
yapo,kwa maana imeandikwa katika , Isaya 3:10 Waambieni wenye haki
ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao
Nina nena na wewe uliye poteza tumaini, wewe
ambaye umeitafuta kazi kwa miaka mingi ukakosa, wewe ambaye madaktari walisema
huwezi kuzaa,wewe ambaye ndugu na jamaa
zako walikufukuza nyumbani sababu ya
shinda, wewe ambaye una matatizo ya ndoa, Mungu anakuja kukuondolea msiba na
matatizo ya maisha yako.
Ndugu zangu msife moyo, lakini muwe na moyo
mkuu, mkijua mateso mnayopitia ni ya muda tu, Kuna utukufu ambao unakungonjea,
Endelea kuliitia Jina la Bwana wa majeshi,
BWANA AWABARIKI SANA
.